JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemteua Bwana Masanja Kungu Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), ambako anakwenda kuchukua nafasi ya Mhandisi Elias Mshana ambaye anastaafu hivi karibuni.

Kabla ya Uteuzi huo Bwana Masanja Kadogosa alikuwa Mkurugenzi Idara ya Mikopo Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB). Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
02 Februari, 2016.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi iakuwaje mtu anateuliwa kukaimu nafasi!!?? Mimi nilidhani ukaimu ni ni automatic kutokutana na position yako. Mfano rais akiwa nje ya nchi, makamu anakaimu, then spika wa bunge and forth. Hata mkurugenzi mkuu ana msaidizi atakayekaimu in case of death,termination or suspension. I could be wrong naomba nielimishwe

    ReplyDelete
  2. Kukaimu hapo ina maana ya "interim", kwamba ni uteuzi wa muda, baadaye atafanya permanent appointment ya full term.

    ReplyDelete
  3. Mdau no.1 uko sahihi kabisa. Kukaimu ni kushika nafasi/ wadhifa kwa muda, mpaka hapo anaetakiwa kuchukua nafasi hiyo atakapopatikana au atakaporudi kwenye nafasi yake. Kwa TRL, management yote ni uozo mtupu, hata wa kukaimu hiyo nafasi hamna bora apelekwe huyo wa muda akutane na changamoto na tunaamini atazitatua, tena na hiyo management yenyewe ingefaa kama ingekaa pembeni kabisa. Uwezo wao wa kufikiri umeshafikia ukingono ndo maana madudu ni mengi ndani ya kampuni hiyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...