Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji, akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuchaguliwa, kwenye Mkutano Mkuu uliokuwa ukifanyika Jijini Mwanza. Dkt. Mashinji anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Aliekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willbload Slaa. 
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA wakishangilia baada ya kupatikana bila kwa Katibu Mkuu mpya, Dkt. Vicent Mashinji.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, Makamu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Mh. Said Issa Mohamed pamoja na Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Mh. Edward Lowassa wakifarilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu mpya wa Chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji (hayupo pichani).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...