Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MGOGORO wa kugombea ardhi ya shamba la Lokolova lenye ukubwa wa ekari 2,470 lililopo kata ya Makuyuni wilaya ya Moshi vijijini umeibuka upya huku wananchi jamii ya wafugaji wakimbebesha lawama mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi hatua yake ya kutangaza kurejeshwa ardhi hiyo kwa chama cha Ushirika wa Wakulima ,wafugaji na uzalishaji mali cha Lokolova.
Mgogoro huo wa zaidi ya miaka 30 sasa ,umeibuka baada ya kundi kubwa la wananchi hao kukusanyika katika eneo hilo wakiwa na mifugo yao pamoja na mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakiimba kuonesha kupinga hatua hiyo ya serikali wakidai itachochea kuibuka kwa mgogoro uliokuwepo.
Februari 19 mwaka huu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Makala akiwa ameongozana na viongozi wengine kutangaza maamuzi ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa kurejesha shamba hilo kwa Ushirika wa Lokolova hatua ambayo imefuta mpango wa awali wa serikali ulioasisiwa na mtangulizi wake (Leonidas Gama) wa kulifanya eneo hilo la ardhi litumike kujenga soko la kimataifa na mji wa viwanda.
Katika mkutano wake wa hadhara na wanachama wa chama cha ushirika cha Lokolova pamoja na wananchi wa eneo hilo Makala aliweka bayana hatua zilizofikiwa na kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichokutana Feb.12 Mwaka huu Mjini Moshi kuwa Serikali imeridhia kurudisha shamba lenye ukubwa wa ekari 2,470 kwa wanaushirika.
Kiongozi wa wananchi Jamii ya wafugaji washio vijiji vya Lotima na Makuyuni Ismail Sevule alisem katika tamko lao kuwa wanapinga hatua ya mkuu wa mkoa (Makala) kurejesha ardhi hiyo ya Shamba la Lokolova kwa chama cha Ushirika ,Ushirika ambao walida ulikwisha futwa tangu mwaka 2014.
“Tunatoa tamko la kupinga hatua ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kurejesha ardhi ya eneo la Lokolova kwa chama cha ushirika ,wanaushirika ambao si wa kata ya Makuyuni ,watu hawa waliingia kwa mbinu katika ushirika uliokuwepo ,hata hivyo bado ushirika huu ulifutwa tarehe 1 4 ,mwezi wa tatu mwaka 2014 na kutangazwa katika gazeti la serikali la tarehe 23/5 mwaka 2014 “.alisema Sevule.
hi hao wakiimba kupinga hatua hiyo.Msemaji wa jamii ya wafugaji Ismail Sevule (mweye kofia ya kijani) akiwa na wananchi.

Wananchi
jamii ya wafugaji wakiwa wamebeba Mabango yenye ujumbe mbalimbali
wakipinga hatua ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala kurejesha
ardhi ya Shamba la Lokolova kwa chama cha Ushirika wa Wakulima ,wafugaji
na uzalishaji mali cha Lokolova.

hi hao wakiimba kupinga hatua hiyo.Msemaji wa jamii ya wafugaji Ismail Sevule (mweye kofia ya kijani) akiwa na wananchi.
Wananchi wakipiga Push Up wakati wa mkusanyiko huo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...