Golikipa mahili wa Mbeya City Fc ya Mbeya, Juma Kaseja  Juma  (pichani) amerejea kikosini kutoa mapumziko ya majuma mawili aliyopewa na kocha  Kinnah Phiri kufuatia  mkewe Bi Nasra Nassor kujifungua watoto mapacha hivi karibuni.
Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa  mbeyacityfc.com  Kaseja amesema kuwa amefurahi kusafiri na hatimaye kurudi salama kwenye timu yake huku pia akitoa shukurani zake za dhati wa wale wote ambao wamekuwa karibu nae yeye kama mchezaji na pia familia yake tangu alipojiunga na City.
“Nashukuru mungu nimefika hapa salama baada ya safari yangu, pia namshukuru kwa kile alichonijaalia, nimerudi kikosini nikiwa na ari kubwa zaidi  ili kuituikia timu yangu kwa nguvu zote  katika kutafuta mafanikio hasa kwenye kipindi hiki  ambacho ligi inaelekea mwishoni, hakika tunapita kwenye kipindi kigumu lakini  umoja wetu utatufanya kuvuka hapa” alisema.
Akiendelea zaidi Kaseja  aliyewahi kucheza kwa mafanikio kwenye timu za Moro United, Simba, na Yanga aliweka wazi kuwa anaimani kuwa na kocha Kinnah Phiri kuwa ataijenga upya City na kuifanya kuwa timu itakayotisha zaidi kwenye msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...