Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.(Picha na Ofisi ya Bunge).
Mkuu
wa Hifadhi ya Saadani Bw. Hassan Nguluma akiwaonesha Wajumbe wa Kamati
ya Maliasili, Utalii na Ardhi ramani ya Hifadhi hiyo wakati kamati hiyo
ilipoitembelea Hifadhi ya Saadani pamoja na kukutana na Menejimenti ya
TANAPA. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili
Mhandisi Ramo Makani (mweye miwani) na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Mhe Atashasta Nditiye.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti ya TANAPA wakati kamati hiyo iliopotembelea Hifadhi ya Saadani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utalii wa TANAPA Bw. Ibrahim Musa akitoa ufafanuzi wa
masuala mbalimbali wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.






Ndugu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya maliasili,Tunaiomba sana kamati yako itufanyie uchunguzi wa waziri wa maliasili na utalii Bwana Magembe,kwa kufanya maamuzi ambayo hata hakufanyia uchunguzi wa kusimamisha biashara ya viumbe hai bila kufuata taratibu,eti kwa kisingizio cha tumbili wanaotoroshwa.sasa imethibitika kuwa yeye kapigiwa simu na mfanya biashara mmoja wa wa kirusi hapa dar es salaam (ambaye ana leseni ya nyara hapa Tanzania) kuwa kuna tumbili wanatoroshwa na hawana vibali bila kufanya uchunguzi ukweli huyu mrusi baada ya kukosa soko la kuuza hao ngedere kwa waholanzi ndio walioshinda tenda Armenia (waliokamtwa) ya kuuza hao ngedere kaamua kuwafanyia fitina kwa kueneza habari za uongo kuwa hawa jamaa hawana vibali wakati wanakila kitu,je waziri anawezaje kumsikiliza mtu tena mfanya biashara binafsi bila kufanya uchunguzi wa kuwashilikisha wataalamu wa wizara yake??? je hawa ndiyo mawaziri wa magufuli wanaokulupuka tu bila kufanya uchunguzi na kujichukulia sheria za kibabe siyo kuwatumikia wananchi walioplipia vibali na bila taarifa anaamua anavyotaka.hii serikali ya wapi isiyofuata sheria mtu anaamua tu
ReplyDeleteBiashara ya Nyara hai ( TDL) INASIMAMIWA NA SHERI YA BUNGE YA WANYAMA PORI NO. 5 YA MWAKA 2009...PAMOJA NA KANUNI ZAKE .
ReplyDeleteINFANYIKA KUPITIA MADARAJA ( CLASSES ) 13,
MOJA YA MADARAJA HAYO NI NO. 13 AMBAYO NI PRIMATES ( NGEDERE,TUMBILI NA NYANI) NA WAMEORODHESHWA AINA ZAKE NA IDADI.....KWA MWAKA TUNARUHUSIWA KUSAFIRISHA PRIMTAES 5000..
PIA PRIMATES HAO NI MOJA YA WANYAMA WAHARIBIFU WA MAZAO WAKUBWA...
BIASHARA HII HUFANYIKA KITAALAMU KUZINGATIA SHERIA ZA TA NZANIA NA ZILE ZA KIMATAIFA ( CITES ), KWANI BIASHARA HII NI YA KIMATAIFA HIVYO HAINA USIRI WA AINA YEYOTE. IPO WAZI....HUFANYWA NA WATU WALIOOMBA LESENI WIZARANI KILA MWAKA KUFUATIA TANGAZO LA WIZARA KAMA SHERIA INAVYOTAKA..NA UKAGUZI HUFANYIKA KUHAKIKISHA WAOMBAJI WANA UWEZO WA KUWATUNZA.
KABLA YA KUKAMATWA WANYAMA HUSIKA LAZIMA WALIPIWE IDARANI TENA KWA THAMANI YA US DOLLAR YA SIKU HIYO, PIA LAZIMA WAPIMWE NA VETERINAY DOCTOR WA SERIKALI NA KUPEWA HEALTH CERTIFICATE HUSIKA..
PIA UASAFIRISHAJI WAKE LAZIMA UZINGATIE SHERIA ZA USAFIRI WA ANGA KIMATAIFA ( IATA- LAR ) BIASHARA HII HUINGIZA SERIKALINI FEDHA ZA KIGENI AMBAZO NI MUHIMU SANA...
mATUMIZI YA WANYAMA HOTE HUSIKA HUFANYIKA KWA KUZINGATIA MATUMIZI ENDELEVU ( SUSTAINABLE UTILIZATION )..ILI KUHAKIKISHA IDADAI YAO HAIPUNGUA NCHINI....VIGEZO VYA KITAALAMU HUTUMIKA.MAMBO HAYA YOTE YAPO WIZARANI KWA KILA MTU ....TATIZO LA SISI WATANZANIA HATUPENDI KUJUA UKWELI , TUNAPENDA MANENO YA BARABARANI YASIYO NA UKWELI.REJEA KWENYE SAKATA LA TWIGA,,,,NANI ALIFUNGWA???
NI VIZURI MKAWA MNAULIZA ILI MUELEWESHWE BADALA YA KUHISI MNAJUA.. NA KUULIZA SI UJINGA...JE MKIJA ELEWA KUWA TATIZO HILI LA NGEDERE LIMEPOTOSHWA NA WATU AMBAO SI WATANZANIA KWA SABABU ZAO ZA KIBIASHARA BINAFSI MTAJISIKIAJE..???
NCHI YETU NI TAJIRI, ILA SISI WENYEWE TUNASHINDWA KUNUFAIKA IPASAVYO KWA SABABU NI RAHISI KUDANGANYWA NA WAGENI....TUNAFIKIRI WAZUNGU WOTE WANAJUA KILA KITU, KWA HIYO KILA ANACHOKUAMBIA MZUNGU TUNAONA NI KWELI..TUSIONEE WATU KWA FAIDA BINAFSI...NDIYO MAANA TUNASISITIZA HUYU WAZIRI WA MALIASILI AMEKULUPUKA TU KWENYE HII SAKATA YA UTOROSHWAJI HAO NGEDERE HABARI HIZI SI ZA KWELI