Na Bashir  Yakub.

Mtu  anaposhtakiwa/kulalamikiwa  hutakiwa  kufika  mahakamani.  Lakini  atafikaje  mahakamani  bila  kujua  kama  ameshitakiwa. Ni  lazima  kuna  utaratibu  wa  kumjuza  mtu  kuwa   kuna  shitaka   dhidi  yako. Na  utaratibu  ambao  hutumika  si  mwingine  bali  ni  kumtumia   mtu  wito  maalum ambao  hujulikana  kama  summons.  

1.UTARATIBU  WA  SUMMONS  KWA   MAKUNDI  MAALUM.
Wito  au  summons  ya  kuitwa  kuhudhuria  shauri  baada  ya  kushitakiwa  hutolewa  kwa  namna  tofauti  kutegemea  na  aina  na  mazingira  aliyomo  muitwaji.  Upo  utaratibu  wa  wa  summons  kwa  mtu  wa  kawaida,  utaratibu  kwa  mtu  aliye  nje  ya  nchi, utaratibu  kwa  mtu  aliye  nje  ya  wilaya  au  mkoa, utaratibu  kwa watumishi  wa  vyombo  vya  ulinzi, utaratibu  kwa  mtu  asiyejulikana  alipo, n.k. Baadhi ya tofauti  hizi  ndizo  zitakazotizamwa  katika  haya makala.

2.  SUMMONS  HUTOLEWA   WAKATI  GANI.
Summons/wito  haitolewi   tu wakati  mtu anapofunguliwa  shauri .  Bali  hutolewa  hata  kwa  mashahidi, hutolewa  kabla  ya  hukumu  kwa  yule  ambaye  hakuhudhuria  kesi ambayo  imesikilizwa  upande  mmoja, hutolewa  kama  ukumbusho kwa  mtu  ambaye  alikuwa  akihudhuria  mahakamani  lakini  baade  akaacha, n.k.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...