Mshindi wa shindano la uvumbuzi wa Teknolojia mpya itakayo saidia jamii kupatikana leo na kuzawadiwa shilingi milioni tano (5,000,000) katika mkutano wa wadau wa teknologia unaofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umeandaliwa na Bites&Bytes ukishirikiana na IBM, TWAWEZA, FSDT pamoja na CBA, mktano huo ambao utahamasisha uendelezaji wa mawazo mapya na uvumbuzi kwa waanzishaji wapya wa biashara na kuwapa mwanya wa kubadilisha mawazo na wadau wengine.
  Baadhi ya wadau wa Teknologia wakimsikiliza  mtoa mada (Hayupo) pichani jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
  Mwakilishi mwenza wa Bits&Bytes,Zuweina Farah akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Teknologia na uvumbuzi wa teknologia mpya itakayo wasaidia wanachini kufanya kazi kwa urahisi zaidi, leo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Amesema kuwa leo washiriki 16 walioshiriki kuvumbua teknoloia mpya wameshiriki katika mkutano huo na ndipo mshindi atakaye fanikiwa kushinda katika shindano hilo atazawadiwa shilingi Milioni 5 kwa kuwa na wazo zuri kuliko wengine ili aweze kuwa na mtaji kwaajili ya kuendeleza uvumbuzi wake.
Mwanafunzi mshiriki wa uvumbuzi wa Teknologia mpya itakayo wasaidia jamii, Gibson Kawago wa shule ya Sekondari ya huko Arusha akiwa amegundua taa za miale ya jua(Solar Power) zinazoweza kuchaji simu za Smati kwa zaidi ya masaa nane.
Baadhi ya washiriki katika mkutano wa Teknologia. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...