Na Grace Michael.

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya zoezi la uhamasishaji wa huduma yake mpya ya Toto Afya Kadi kwa kutoa elimu ya namna ya kujiunga na kunufaika na huduma hiyo pamoja na kugawa vipeperushi vinavyoelezea huduma zinazotolewa na Mfuko.

Zoezi hilo limeongozwa na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Athumani Rehani ambapo maofisa wa Mfuko walihudumia wananchi mbalimbali katika barabara ya Kilwa.

Huduma ya Toto Afya Kadi inalenga kuhudumia watoto ambao ni chini ya umri wa miaka 18 ambao watajiunga na Mfuko kwa gharama ya shilingi 50,400 kwa mwaka ambapo watapata huduma za matibabu kutoka kwenye kitita cha Mfuko.

Akizungumza na wananchi mbalimbali, Bw. Rehani aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kwa lengo la kuondoa tatizo la kukosa matibabu kwa watoto ambao wengi wameonekana kukosa matibabu wakati wanapougua.

“Hii fursa ni kwa ajili ya watoto kundi ambalo ni kubwa na ni la muhimu kuhakikisha linakuwa kwenye mazingira mazuri ya uhakika wa matibabu hivyo wananchi ni wakati umefika wa kuwaweka watoto katika mazingira mazuri ili waweze kutimiza ndoto zao,” alisema Bw. Rehani.

Kwa upande wa wananchi walipongeza kitendo cha NHIF cha kuingia mtaani kuwafuata wananchi na kuwapatia elimu ya huduma wanazotoa kwa kuwa hatua hii itasaidia watu wengi kuanza kutumia fursa zilizopo.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Rehani Athuman akiongoza zoezi la ugawaji vipeperushi vya huduma mpya ya Toto Afya Kadi katika Barabara ya Kilwa leo.
Meneja Masoko na Elimu kwa Umma Anjela Mziray akitoa elimu ya Afya Toto Kadi
Mafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakiendelea na zoezi.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...