NMB Mdhamini Mkuu wa
Mkutano Mkuu wa ALAT taifa.
Benki ya NMB imekabidhi hundi ya
mfano ya shilingi Milioni 100 kwa uongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa
Tanzania (ALAT) kwaajili ya udhamini wa mkutano mkuu wa ALAT taifa unaotarajia
kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa Aprili Mjini Dodoma.
Fedha hizo ni kwaajili ya
kugharamia gharama za mkutano mkuu unaotarajia kukutanisha wajumbe zaidi ya 400
kati yao wakiwa mameya 180 kutoka halmashauri zote nchini, wakurugenzi wa
halmashauri wapatao 180, wawakilishi wa mikoa na wizara mbalimbali ambao jumla
yao wanafika zaidi ya 400.
NMB imekuwa ikidhamini mikutano
ya ALAT kila mwaka na kwa mwaka huu, malengo makubwa ni kuhakikisha halmashauri
zote zinaingia kwenye mfumo wa malipo ya kielektroniki ili kuzuia upotevu wa
mapato. NMB kama mpokeaji mkuu wa malipo kwa njia za kielektroniki kwenye
halmashauri, tayari imeshafanya majaribio ya kupokea malipo kwa njia hizo na
hivi karibuni itaanza kutoa huduma hiyo kwenye halmashauri zote nchini.
Kupitia mtandao wake wa matawi
180 nchini, NMB imekuwa karibu na wananchi wa halmashauri mbalimbali kwa kutoa
huduma za kifedha na pia kusaidia serikali katika uboreshaji wa njia za
ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki.
Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na
Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa akikabidhi mfano wa hundi ya
Shilingi milioni 100 kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania
(ALAT), Habraham Shamumoyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mshauri wa
Mawasiliano-ALAT, Seif Hassan. NMB imedhamini mkutano mkuu wa ALAT unaotarajia
kufanyika mapema mwezi April mjini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala
za Mitaa Tanzania (ALAT) Habraham Shamumoyo akiongea na waandishi wa habari
(hawako kwenye picha) kuhusu Mkutano Mkuu wa Tawala za Mitaa utakaofanyika
jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya
NMB - Richard Makungwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...