Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha inawasaidia wakulima kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanaonekana kuendelea kuikabili nchi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) na Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN) ili kujadili mpango wa Kilimo Salama (CSA).
Bi. Natai alisema serikali inatambua uwepo wa mabadiliko ya Tabia ya Nchi na kwasasa tayari wataalamu wanafanya tafiti ili waone ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia wakulima kupambana na mabadiliko hayo.
Alisema kwa sasa bado wakulima wengi hawajafahamu kama kuna mabadiliko ya tabia ya nchi na hivyo wamekuwa wakitumia njia za asili lakini baada ya utafiti watapatiwa mbinu mpya za kupambana na mabadiliko ambapo wataweza kutumia njia za kisasa ambazo zinaonekana kuwa bora zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi.
Wageni
rasmi katika mkutano huo, Wa kwanza kushoto ni Mtafiti kutoka Taasisi
ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili
(FANRPAN), Njongenhle Nyoni, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti
wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida na Mkuu wa Kitengo cha
Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande
Natai.
Mshereheshaji wa mkutano huo akiwakaribisha wageni waalikwa kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo.
Baadhi ya wageni waliohudhuria katika mkutano huo kujadili mpango wa Kilimo Salama (CSA).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...