Wakazi wa mji wa Sumbawanga watakiwa kuchukua taadhari juu wa ugonjwa wa mlipuko wa Kipindupindu ili kuepukana na madhara ya ugonjwa huo.

 Watu zaidi ya Sita wanaripotiwa kuwa na ugonjwa huo na wamefikishwa katika hospitali ya mkoa wa Sumbawanga kwajili ya matibabu.

 Serikali ya mji huo wa Sumbawanga imewataka wakazi wote wa mji huo kuchukuwa taadhari juu ya ugonjwa huo kwa Kunawa mikono yao kabla ya kula chakula na baada ya kula na 
 kufanya usafi wa mazingira.

Pia wameaswa kuwakataza watoto wao kucheza katika mitaro ambayo haitiririshi maji machafu (inayotuamisha maji) na tahadhari zinginezo kujikinga na Ugonjwa huo uliopo hivi sasa Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...