Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona wa tatu kulia akiwa anaonyeshwa moja ya madini ya vifo yalioletwa katika maonyesho ya wafanyabiashara wa ndani wa madini hayo yaliyofanyika ndani ya mji mdogo wa mirerani mkoani Manyara
Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer akiwa anaonyesha jiwe la Tanzanite ambalo lipo tayari kuuzwa.
Idha benki ya NMB ilimefungua rasmi tawi katika mji huu ndogo wa mererani hapa meneja wa mji mdogo wa benki hiyo akiwa anamueleza mkuu wa wialaya pamoja na wananchi waliouthuria semina hiyo huduma ambazo wanazitoa benki hiyo ndani ya mji mdogo wa mirerani
Mkuu wa wilaya akiwa anakata utepe hii ikiwa ni ishara ya kufunguliwa rasmi kwa maonyesho hayo ya vito na madini.
MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaagiza 
wote waliovamia na kujikatia viwanja au kujenga kwenye eneo huru la 
usafirishaji bidhaa nje (EPZA) waondoke na kubomoa kabla hawajaondolewa kwa 
nguvu. 

Inadaiwa kuwa vigogo watatu wa mji mdogo wa Mirerani, wamejenga nyumba za 
kuishi kwenye eneo hilo na watu wengine zaidi ya 11 wamejimegea viwanja 
kiubabe na kujiandaa kujenga ili hali mradi huo unatarajia kuanza kujengwa. 

Akizungumza juzi wakati akifungua maonyesho ya madini ya vito ya siku
mbili yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani, Kambona alisema mchakato wa
kuwalipa fidia waliokuwa wanamiliki eneo hilo upo tayari hivyo wavamizi hao 
waondoke. 

Alisema baada ya kuwalipa waliokuwa wamiliki wa eneo la EPZA, mchakato wa 
ujenzi utaanza mara moja kwani kutajengwa kituo kikubwa cha biashara za 
kuuza nje ikiwemo soko la madini ya Tanzanite litakalojengwa sehemu hiyo. 

Hata hivyo, alipongeza Wizara ya Nishati na Madini kufanya maonyesho hayo 
kwa mara ya kwanza kwenye mji mdogo wa Mirerani, sehemu yanapopatikana 
madini ya Tanzanite, kwani itasaidia kuboresha soko la madini katika eneo 
hilo. 

“Ni heshima kubwa tumepatiwa watu wa Simanjiro hususan mji mdogo wa
Mirerani, hivyo tutumie fursa hii kwa wachimbaji kuleta madini yetu kwenye
maonyesho haya ili kuboresha uchumi wetu,” alisema Kambona. 

Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer alisema
maonyesho kama hayo yanachangia kutangaza madini hayo, kwani kuna baadhi ya 
watu wana dhana potofu kuwa yanachimbwa nchi ya jirani. 

“Kupitia maonyesho haya tunaiomba serikali iboreshe zaidi sekta ya madini
ya vito kwa kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo kwani wana changamoto 
nyingi zinazowakabili,” alisema Laizer. 

Kwa upande wake, kaimu kamishna wa madini kanda ya kaskazini Elias
Kayandabila alisema maonyesho hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mji mdogo 
wa Mirerani na yanatarajia kufanyika tena mwakani kwenye eneo hilo. 

Kayandabila alisema kupitia maonyesho hayo wafanyabiashara wadogokwa
wakubwa wa madini ya vito ikiwemo Tanzanite, Tomarine ya kijani, Garnet ya
kijani, Roadlite na mengineno, watanufaika nayo kwa kuboresha masoko yao. 

Maonyesho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Nishati na Madini 
kanda ya ya kaskazini na vyama vya wachimbaji madini (Remas), chama cha 
madalali wa madini (Tasgedo) na chama cha wauzaji wa madini (Tamida).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...