Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, ni Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa March. Miongoni mwa majukumu ya Mwenyekiti wa Mwenzi ni pamoja na kuitisha , kuratibu na kuendesha mikutano inayowahusisha Wawakilishi wa Kudumu kutoka Nchi 53 wanaoziwakilisha Nchi zao katika Umoja wa Mataifa.
Mwenyekiti wa mwezi, pamoja na kuratibu na kuendesha mikutano yenye ajenda mbalimbali pia anawajibika katika kuwasilisha kauli ya nchi za Afrika kupitia ama utoaji wa hotuba au mawasiliano na Wakuu wa Idara mbalimbali ndani ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa, akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pale inapolazimu.
Pichani ni baadhi ya Matukio yaliyotokea mwishoni wa wiki wakati wa Mkutano wa Wawakilishi hao wa Nchi za Afrika chini ya uenyekiti wa Tanzania, ambapo walipokea taarifa mbalimbali kutoka kwa watendaji wa Umoja wa Mataifa pamoja na taarifa kutoka kwa Muungano wa Wakuu wa Idara za Takwimu kutoka Afrika waliokuwa wakishiriki katika Mkutano wa 48 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.
Balozi Tuvako Manongi akimkabidhi zawadi ya kumuanga kwa niaba ya Mabalozi wenzie aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Liberia katika Umoja wa Mataifa, Balozi Marjon V. Kamara ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Liberia.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dr. Albina Chuwa (kushoto) akitoaa taarifa fupi kwa niaba ya Wakurungezi Wakuu wa Idara za Takwimu kutoka Nchi za Afrika kuhusu maazimio na mapendekezo yao kuhusu viashiria vya ajenda ya Maendeleo Endelevu. Kulia kwa Balozi Tuvako Manongi ambaye Tanzania ni Mwenyekiti wa Mwezi wa nchi za Kundi la Afrika ( African Group) Ni Mtakwimu Mkuu kutoka Ivory Coast.
Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi wa Idara ya Siasa ya Umoja wa Mataifa, Bw. Taye-Brook Zerihoun naye akiwasilisha taarifa yake kwa Wawakilishi wa Kudumu wa Nchi za Afrika, ambapo pamoja na mambo mengine aliwaomba wawakilishi hao kuunga mkono pendekezo la Idara yake la kupatiwa fedha ambazo wanataka kuzitumia katika eneo la uratibu na usimamia wa majadiliano kuhudu dhana nzima ya uzuiaji wa machafuko ( mediation and prevention ) pamoja na kuongeza ajira.
Sehemu ya Mabalozi na Maafisa kutoka nchi Wanachamawa Umoja wa Afrika wakifuatilia mkutano.
Sehemu ya Mabalozi na Maafisa kutoka nchi Wanachamawa Umoja wa Afrika wakifuatilia mkutano.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...