NA KHAMISI MUSSA

CHAMA cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), kinatarajia kufanya matembezi katika shule mbalimbali za watoto wenye mahitaji maalum zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya kinywa na meno.

Hayo yalisemwa na Rais wa TDA, Dk. Lorna Carneiro, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo alibainisha kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni 'afya njema ya kinywa ni afya ya mwili mzima'.

Dk. Carneiro, alisema Machi 14 hadi 19 madaktari watatembelea shule ya mahitaji maalum ya Mtoni Maalum, Sinza Maalum, Buguruni Maalum na zingine za Mkoa wa Morogoro ambapo pia watafanya uchunguzi na matibabu.Alisema katika siku ya 
kilele TDA itatoa huduma ya uchunguzi wa kinywa na meno kulingana na mahitaji katika Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege ambapo mgeni rasimi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Rais huyo alisema pia chama hicho kitatoa elimu, uchunguzi na matibabu ya kinywa na meno kwa waototo wenye ulemavu wa ngozi walioko Buhangija Shinyanga.


  Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro akifungua mkutano huo

 Mkuu wa Idara ya Meno, Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk, Rachel Mhavile akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya  Maadhimisho ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani yatakayofanyika mkoani Morogoro Machi 20,mwaka huu.kushoto ni Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Ambege Mwakatobe.
  Mkuu wa Huduma za Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto  Dr. Ahadiel Senkoro, akizungumza jambo katika Maadhimisho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...