Kwa mara ya kwanza, wadau wa Sanaa nchini wamepata fursa ya kukutana na Makampuni, Mashirika na Vyombo mbalimbali katika mafunzo yaliyofanyika hotel ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam. Semina hii iliongozwa na Maria Sarungi Tsehai, ambaye ni mdau mkubwa katika sekta hii
Mafunzo hayo yalifanywa na wataalam kutoka sekta mbalimbali kama Nyumba, Urembo, Saikolojia, Sanaa na Wasanii n.k
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba, Arden Kitomari,akitoa mafunzo ya namna ya kuwekeza katika Sekta ya Nyumba nchini Tanzania,hususan kupitia miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa
Wadau wa Sanaa pia walipata mafuzo ya Namna ya kubalansi maisha yao ya Sanaa na yale ya Familia, kutoka kwa mwanasaikolojia maarufu, Aunt Sadaka Gandi.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...