Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa, Hiiti Sillo akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kukamatwa kwa kiwanda bubu cha kutengeneza perfumes bandia aina SAME.leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo akiwaonesha wandishi wahabari (hawapo pichani) mitambo ya kutengenezea perfumes bandia zinazoitwa kwa jina la SAME leo jijini Dar es Salaam.
Wandishi wakimsilkiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa, Hiiti Sillo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA), Hiiti Sillo akiwaonesha wandishi wa habari perfumes bandia zinazoitwa kwa jina la SAME leo jijini Dar es Salaam.
Na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ,Kanda ya Mashariki kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imekamata vipodozi vya manukato ‘Perfume’ katika nyumba inayomilikiwa na Mwanaidi iliyopo eneo la Tuangoma, Wilayani Temeke Mkoani Dar es Salaam.
Akizungumzna na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo ,Mkurugenzi Mkuu wa TFDA,Hiiti Sillo amesema kuwa walipata taarifa juu ya utengenezaji wa mafuta ya manukato na ndipo wakafanyia kazi na kwenda kukamata.
Amesema katika nyumba hiyo ina vifaa vya kimaabara, malighafi na kemikali mbalimbali za kutengeneza manukato yenye alama ya kibiashara SAME huku mafuta yakionyeshwa stika kuwa inatengenezwa nchini Uturuki
Sillo amesema wangalizi wa nyumba hiyo Fatuma Selemani anashikiliwa na Jeshi la Polisi ili kusaidia upelelezi na jalada la Polisi na MBL/IR/1998/2016 limefunguliwa katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbagala, Temeke.
Amesema vielelezo vyote ikiwa ni chupa 5,350 za perfumes zilizokamatwa dukani pamoja na vifaa, malighafi, kemikali na stika mbalimbali zilizokamatwa dukani vinashikiliwa.
Sllo amewaomba wananchi wote ambao wanazo majumbani kwao perfumes aina ya SAME waache kuzitumia na wazirudishe katika ofisi za TFDA zilizopo hapa nchini kwa sababu perfumes hizo hazijasajiliwa na TFDA na hivyo ubora na usalama wake haufahamiki.
Aidha amesema wananchi waendelee kutoa taarifa kuhusu mtu au makundi ya watu mbalimbali wanaojihusisha na biashara haramu za utengenezaji, uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba katika maduka au majumbani mwao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...