Mkurugenzi wa kampuni ya simu ya TTCL nchini Dk Kamugisha Kazaura akimuelekeza jambo Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliani Professa Makame Mbawala kuhusu mkongo wa mawasiliano uliopo mpakani mwa Tanzania na Burundi. 
Vijana waliokutwa na nyaya za wizi za kampuni ya TTCL waliokamatwa usiku wa kuamkia leo na wanachi (kushoto) Haroon Khamani na Amos khalidi.

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wilaya ya Kasulu juu ya wezi wa nyaya za simu za kampuni ya TTCL kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria haraka kwa kuhujumu mawasiliano.
  Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu za TTCL nchini Dk Kamugisha Rwezaura akiongea na vyombo vya habari juu wezi waliokata nyaya za simu TTCL mtaa wa Sovya Wilayani Kasulu

Editha Karlo, Kasulu

WANANCHI  wa Mtaa  wa soko la sovya Wilayani Kasulu usiku wa kuamkia leo wamewakamata wezi waliokuwa wamekata nyaya za mawasiliano za kampuni ya TTCL.

Akiongea juu ya tukio hilo Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu TTCL nchi Dk Kamugisha Kazaura alisema kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la soko la sovya majura ya saa kumi na moja alfajiri. Alisema kuwa wananchi  wanaoishi karibu na eneo lililokatwa nyaya hizo ndiyo waliowakamata vijana hao baada ya kufanya uhslifu huo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa hasara waliyoipatia kampuni kwa kukata nyaya hizo inakadiliwa ni zaidi ya milioni 20.

"Hasara waliyoingizia serekali ni kubwa sana hizo nyaya walizokata zinagharimu milioni 20,lakini kuitengeneza upya line hiyo inaweza kugharimu zaidi ya hiyo fedha''alisema Kazaura

Alisema kutokana na wezi huo umepelekea baadhi ya ofisi za serekali kukosa mawasiliano ikiwemo ofisi ya polisi Wilaya,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Bank na Takukuru. Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano profesa Makame Mbawala alivitaka vyombo vya dola kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wezi hao wanaohujumu mawasiliano.

"Hawa muwapeleke kwenye sheria hiki walichofanya ni kosa kwa sheria ya mwaka 2015 wanatakiwa kulipa faini isiyopungua milioni 50 au kifungo jela ili iwe fundisho kwa wengine"alisema profesa Mbawala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...