Ipo namna nzuri
ya umiliki wa
ardhi wa pamoja
ambayo huepusha migogoro
hasa kwa walio
katika ndoa. Migogoro ya
ardhi hutokea kwa
namna tofauti. Ipo inayotokea
wakati wa uhai
wa wamiliki na
ile itokeayo baada
ya uhai wa wamiliki
wote au mmoja
wao .
Umiliki kwa mafungu
yasiyogawanyika huwa ni
suluhu kwa yote haya. Ni
suluhu kwa wanandoa wenyewe
wanapogombea mali lakini
ni suluhu wakati ndugu
wanapotaka kumpokonya mwanandoa
ardhi iliyoachwa na
mwenza wake baada ya
kifo.
Ni vema
kujua kuwa sheria ya
ardhi kawaida inatambua
umiliki wa ardhi
wa aina mbili.
Tumewahi kueleza umiliki
huo hapa lakini
leo pia tutaeleza.
Upo umiliki binafsi
na umiliki usio
binafsi kwa maana
ya umiliki wa
zaidi ya mtu
mmoja.
1.UMILIKI BINAFSI.
Umiliki binafsi ni
umiliki wa mtu mmoja. Kama
ni nyumba, shamba au
kiwanja kinakuwa chini
ya jina la
mtu mmoja. Huyo
mwenye jina linalosomeka
ndiye huhesabika kama
mmiliki wa pekee.
Haki zote
zikiwemo zile za
kuhamisha, kuweka rehani, kuuza,
kugawa humhusu mtu
mmoja pekee. Hahitaji ridhaa ya
mtu mwingine katika kutekeleza
muamala wowote katika
umiliki huu labda yawepo
mazingira maalum.
2. UMILIKI
WA PAMOJA .
Huu ni umiliki
wa pamoja kama
neno lenyewe lilivyo.
Kwa jina la kitaalam
hujulikana kama “co-occupancy”. Watu wawili
au zaidi huweza
kumiliki nyumba, shamba au
kiwanja kwa pamoja. Haki
za msingi kama
zile za kuhamisha
umiliki, kuuza, kuweka rehani,kutoa zawadi huwahusu
wamiliki wote.
KUSOMA ZAIDI
sheriayakub.blogspot.com



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...