Mwanasaikolojia Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma yanayoendeshwa na Taasisi ya Manjano Foundation yanaoendelea kwenye ukumbi wa LAPF House.

Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Dodoma wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano Foundation na mkufunzi wa maswala ya Biashara mjini Dodoma yanayoendelea kwa wiki nzima.
 Washiki Kutoka Mkoani Dodoma na Maeneo Jirani wakiliskiliza kwa Makini Wakati wa Mafunzo hayo Leo.

Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani, wajiamini, watambue vyeo vyao katika familia, wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.
Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mjini Dodoma kuchangamkia FURSA zinazowazunguka. Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Dodoma kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira. 
Picha ya Pamoja Washiriki hao kutoka Mkoani Dodoma wakiwa na Mwanasaikolojia Anti Sadaka Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions africa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser.

Anti Sadaka amewashauri wanawake wasiache kujifunza na waache kujibweteka baada ya mafunzo haya kuisha isipokuwa wawe makini kutafuta elimu zaidi ya kujiongezea ujuzi katika kazi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...