Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Chemba amekutana na
kufanya mazungumzo na Balozi wa Ireland nchini
Tanzania Bi. Fionnuala Gilsenan ofisini kwake katika jitihada zake za kuinua
sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Waziri
Nchemba alimweleza Balozi huyo kuhusu hali ya sekta ya kilimo na mikakati ya
serikali katika kukabiliana na changamoto zinazokikumba kilimo chetu hapa
nchini ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa mbegu, ambapo vituo vya utafiti vya
serikali na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) vimejikita katika kutafiti
mbegu mbali mbali. “Serikali
imejipanga kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima wetu”
alieleza Mhe. Chemba.
Pia
alisema kuwa uzalishaji wa mbegu bora na hasa za viazi utasukumwa kwa kutumia
kilimo cha umwagiliaji ili ziweza kupatikana kwa wakati kwa wakulima wetu. Upatikanaji
wa uhakika na kwa wakati wa mbolea kwa wakulima ni moja ya mikakati ya Serikali
katika kuboresha na kuinua kilimo.
Mikakati mingine kwa mujibu wa Waziri Nchemba ni kwa upande sekta ya mifugo ambapo kuna changamoto ya kuwabadilisha wafugaji kutoka ufugaji wa kiasili na kuingia katika ufugaji wa kisasa.
Jitihada
nyingine ni kuwaingiza vijana katika ufugaji wa kisasa wa samaki kwa
kuwawezesha kupata zana bora za uvuvi, alibainisha Mhe Nchemba.Balozi
Bi. Gilsenan alimfahamisha Waziri Nchemba kuwa nchi yake imedhamiria kusaidia
kuinua tija kwa kuboresha mnyororo wa thamani ya mazao.Sehemu
nyingine muhimu kwa mujibu wa Bi. Gilsenan ni pamoja na huduma za ugani,
hifadhi na matumizi bora ya ardhi yanayolenga kupunguza migogoro, na kuchochea
upatikanaji wa masoko kwa mazao yanayozalishwa.
Naye
Mratibu wa Kitengo cha Mahusiano na Misaada ya Kimataifa kwa Wizara ya Kilimo
Mifugo na Uvuvi Bi. Margareth Ndaba ameainisha maeneo ambayo Ireland inaweza
kusaidia kuwa ni pamoja na lishe, Kilimo cha mboga mboga, zana za kilimo,
utafiti na viwanda vya maziwa ili kusaidia kuondoa umaskini kwa Watanzania.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Mifugo , Tanzania Dkt. Furaha
Mramba alianisha changamoto ambazo Ireland inaweza kusaidia katika kuendeleza
mifugo kuwa ni mabadiliko ya tabianchi ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa
katika kuibua magonjwa mapya ya mifugo.
“Tunaomba
Ireland kusaidia katika chanjo za mifugo ili kupambambana na magonjwa
yanayoambatana na mabadiliko ya tabianchi” , alisisitiza Dkt Mramba.Wakati
huo huo Waziri Nchemba alikutana na wadau wa kilimo cha viazi kutoka Finland
wakiongozwa na Naibu Balozi wa Finland nchini, Bwana Simo – Pekka Parviainen
ambapo walimweleza nia ya kutaka kujikita katika kuboresha kilimo cha viazi
mviringo.
Naye
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Peruna Mestant Bwana Aero Pisila alimfahamisha
Waziri kuwa tayari wametembelea Mkoa wa Mbeya, Njombe na Arusha ili kuona fursa
ya kuinua kilimo cha viazi mviringo na hasa kwa vijana wa Tanzania.
Aidha,
Mratibu wa Mradi wa Kuendeleza kilimo cha Viazi Mviringo hapa nchini Bi.
Matilda Byanda alifamweleza Waziri kuwa tayari wamefanya ziara za
kujitambulisha katika Mikoa husika na kuonana na viongozi wa serikali na
watalaam wa kilimo katika ngazi za halmashauri na kanda husika.
Waziri
Nchemba aliwataka kubainisha maeneo ambayo serikali itachangia katika kutimiza
lengo hilo la kuboresha kilimo cha viazi mviringo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...