Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula kufuatia tukio la mmoja wa Madaktari kupigwa na mwananchi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akemea tabia inayotaka kujengeka ndani ya jamii ya kuwashambulia watumishi wa afya hasa Madaktari na Wauguzi.

Amevitaka vyombo ya dola kuwachukulia hatua wananchi wanaojihusisha na vitendo hivi ambavyo vitaathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa wa kipato cha chini.

Mhe Ummy amewasili Mtwara jana akiongozana na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi ambapo alifanya mazungumzo na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.

Amewaonya wananchi kutoitumia vibaya dhamira ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli na Serikali ya kuimarisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa kujichukulia sheria mkononi.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wazee aliyefika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula mara baada kuwasili hospitalini hapo kuzungumza na wafanyakazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...