Na
Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan
itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh.
Bilioni 116.4 za Kitanzania.
Akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia
katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.
Dkt. Likwelile
alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara,
kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa
ajira nchini.
Mkataba wa pili unahusu masuala ya kiufundi yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya
mkataba uliosainiwa Octoba 20, 1966, kwa
kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano
itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika
kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.
Aidha, makubaliano
hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo
kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya
wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini
Tanzania.
Katibu Mkuu Dkt.
Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo
zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.
Naye Balozi wa Japan
nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani
kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya
uchumi na kijamii.
Balozi Yoshida
amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa
na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri
yanayovutia wawekezaji kuwekeza nchini
Tanzania.
Adha amesema kuwa
Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya
kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya
vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500.
Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akibadilishana hati
ya makubaliano walizosaini na Serikali ya Japan utakaoitakayoiwezesha Tanzania
kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia
ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.
Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akisaini hati
ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar
es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa
na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania
Bw. Masaharu Yoshida.
Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha
Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za
Kitanzania.
Balozi wa Japan
nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania
na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata
kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.(Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO).






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...