Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Melchior Temu (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2015 mbele ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria katika kikao kilichofanyika leo (30/3/2016) jijini Dar Es Salaam. Wengine katika picha ni viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria akiwemo Waziri Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye suti ya kijivu) na wajumbe wa Kamati hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (aliyesimama) akielezea jambo katika kikao cha Viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika leo (30/3/2016) kwenye ukumbi wa Tume ya Kurekebisha Sheria jijini Dar Es Salaam. Kulia kwa Prof. Mchome ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...