Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin (mwisho kushoto) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi wakikabidhi msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe kutoka kampuni ya Zantel. Wanaopokea mwisho kulia ni msanii Aslay na Meneja wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Yusuph Chambuso.
 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa akikabidhi msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi akifuatiwa na mwanamuziki kutoka bendi ya Yamoto, Aslay.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa wa hafla fupi ya makabidiano ya msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe kutoka kampuni ya Zantel. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akifuatiwa na Meneja wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Yusuph Chambuso. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia tukio hilo la Kampuni ya Zantel kukabidhi msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe

Kampuni ya simu ya  Zantel  leo imetoa msaada wa kompyuta 3 na huduma ya intaneti bure kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe kwa ajili ya kuwasaidia vijana walio katika kituo hicho kuweza kunufaika na kazi zao kupitia mfumo wa digitali utakaowawezesha kukuza na kusambaza kazi zao.

Kituo cha Mkubwa na Wanawe ni kituo cha kukuza sanaa, kilichoanzishwa mwaka 2011 katika wilaya ya  Temeke kwa lengo la kufanya maonyesho ya sanaaa na kutoa fursa kwa vijana wanaoishi  kwenye mazingira magumu kuweza  kukuza na kuviendeleza vipaji vyao.Kwa sasa kituo hicho kina idadi ya zaidi ya vijana 102 ambao wana vipaji mbalimbali kama kuigiza,kuimba na kucheza ngoma.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel,Bwana  Benoit Janin amekipongeza kituo cha Mkubwa na Wanawe kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuwasaidia vijana wengi kutimiza ndoto zao na hivyo kuweza kuendesha maisha yao.‘Sanaa ni ajira kama zilivyo ajira nyingine, na sisi kama Zantel tunaamini msaada huu utawawezesha vijana wengi zaidi kuweza kuboresha na kusambaza zaidi kazi zao za sanaa hivyo kuweza kujikimu kimaisha na kutoa  ajira kwa wenzao' alisema Benoit.

Akielezea zaidi kuhusu msaada huo, Benoit aliwataka wasanii walio katika kituo cha Mkubwa na Wanawe kutumia vizuri vifaa hivyo kuendeleza zaidi vipaji vyao.Pamoja na msaada huo, Zantel pia itaandaa utaratibu wa mafunzo ya kompyuta na digitali kwa vijana ili kuwawezesha kupata ufanisi  na ujuzi katika  kukuza na kuendeleza  vipaji vyao. 

‘Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na kituo cha Mkubwa na Wanawe katika utekelezaji wa sera ya taifa ya utamaduni inayosisitiza ukuzaji wa sanaa na hivyo kukuza na kuendeleza maslahi ya wasanii’ alisema Mgeni Rasmi wa hafla hiyo, Bi Leah Kihimbi ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

Naye mwanzilishi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella alitoa shukrani kwa kampuni ya simu ya Zantel kwa kuwatambua uwepo wao na kuwaunga mkono akisema hii ni mara ya kwanza kwa kituo chake kupata msaada kutoka kwa wadau.‘Kituo chetu kinaona fahari kupokea msaada huu ambao utasaidia vijana wetu na kuwapa fursa ya ya kugundua vipaji vilivyojificha  na kuviendeleza  kwenye tasnia hii ya sanaa pamoja na kujitangaza zaidi kazi zetu’ alisema Fella.

Tangu kuanzishwa kwake, Mkubwa na  Wanawe imefanikiwa kuibua wasanii mbalimbali kama vile Wanaume TMK na bendi ya Yamoto.‘Kama Mkubwa na Wanawe tumejikita katika kujenga na kuhakikisha vijana wanatimiza ndoto zao na pia kuwasaida wasishawishike au kujishuhulisha na shughuli haramu ambazo zinapotosha maadili kwenye jamii kama vile uvutaji au suuzaji wa madawa ya kulevya na wizi’ alimaliza Fella.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...