Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Alfred Lucas kuwa Afisa Habari na Mawasiliano mpya wa shirikisho kuanzaia leo Aprili 27, 2016.

Alfred anachukua nafasi ya Baraka Kizuguto aliyehamishiwa katika Kurugenzi ya Mashindano kuwa Afisa Mashindano na Meneja wa Mifumo pepe ya Usajili (TMS).

Alfred ana uzoefu kutoka vyombo mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri.Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari, uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na lugha.
Mawasiliano ya Afisa Habari,

Alfred Lucas:
Namba ya simu: 0769 088111

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...