Wiki iliyopita Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC, alimkaribisha Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete nyumbani kwake kwa chakula cha jioni na kujumuika pamoja na ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao walikuwa nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria mikutano ya Benki ya Dunia (World Bank Group) na International Monetary Fund (IMF) tarehe 12 - 17 Aprili 2016. Kwenye ziara yake jijini Washington, Mhe. Rais Mstaafu Kikwete alishiriki katika Kongamano la Kimataifa la Afya (World Health Congress) na Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kushauri Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya Elimu kwa Wote Duniani (International Commission on Financing Global Education Opportunity).
Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete akiwa katika mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Nduru, wakati alipokutana nao nyumbani kwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson M. Masilingi.
Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, wakiwa kwenye Meza kuu na Mwenyeji wao, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson M. Masilingi na Mkewe Mama Marystella Masilingi.
Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete akizungumza machache wakati akitoa shukrani kwa Balozi Wilson Masilingi, kwa ukaribisho wake.
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania uliopo nchini Marekani kwa Shughuli mbalimbali, wakimsikiliza Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete .
Rais Mstaafu, Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete akibadiliashana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Servacius Likwelile (kushoto), Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu nyumbani kwa Balozi , Tanzania House Bethesda, MD.
Mhe. Rais Mstaafu Dkt. Jakaya M. Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na wenyeji wao, Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Mama Marystella Masilingi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...