Ankal akiwa na furaha na heshima kukutana na magwiji wa ndondi nchini Tanzania leo. Habibu Kinyogoli "Master" (kati) na Emmanuel Mlundwa "Mzee wa Ulaya" jijini Dar es salaam leo.
-----------------------
Kwa wasiowafahamu Mlundwa alikuwa kwenye timu ya Tanzania ya Olympic mwaka 1980
huko Moscow, Urusi (BOFYA HAPA) ambako alifanya vyema. Mlundwa pia
ndiye muasisi wa ndondi za kulipwa nchini
Kinyogoli alinyakua medali
ya shaba katika Olympic mwaka 1972 uzito wa wa Unyoya ama Featherweight (BOFYA HAPA) Mjini Munich, Ujerumani
Kinyogoli ndiye aliyekuwa bondia wa pili wa Tanzania kuleta medali ya
mashindano yanayoshirikisha nchi kutoka nje ya Afrika Mashariki wakati
alipopata medali ya fedha katika Michezo ya Pili ya Afrika (2nd All African
Games) iliyofanyika mjini Lagos, Nigeria mwaka 1973.
Hadi wakati huo mwanamasumbwi aliyekuwa ameleta
medali kutoka nje ya mipaka ya Afrika Mashariki alikuwa marehemu Titus Simba,
ambaye alipata medali ya kwanza ya fedha kwa Tanzania katika Michezo ya Jumuiya
ya Madola mwaka 1970 huko Scotland.
Miongoni mwa mabondia ambao ni matunda
yake ni Majuto Mchevu, aliyemfundisha mwaka 1969 katika klabu ya Magomeni
Community Centre, Zakaria Yombayomba, Habibu Mzungu, Bakari Selemani, Kweli
Msigili, Abbas Pazi, Francis na nduguye Benedict Kakokele aliowafundisha mwaka
1971.
Mwaka 1973, aliweka historia nyingine kwa Tanzania baada ya kushiriki
Michezo ya Pili ya Afrika nchini Nigeria. Katika robo fainali alimpiga bondia
kutoka Madagascar na katika nusu fainali akamtwanga bondia kutoka Mali na
kusonga mbele kwenye fainali kuwania ubingwa wa uzani wa Bantam, ambapo
alikumbana na Omollo wa Uganda aliyemshinda Kinyogoli kwa pointi na hivyo
Mtanzania huyo kuambulia medali ya fedha.
Katika klabu ya Urafiki mwaka 1973 aliwafundisha akina Charles Mhilu 'Spinks',
Lazaro Makali, Salum Temianga, Herbert Sempoli na Mmasi, ambao walikuwa
wakifanyia mazoezi Peninsula Hotel.
Baada ya kustaafu ndondi za ridhaa mwaka 1978 na
kuanza kufundisha watoto ndipo alipopata nafasi ya kuwafundisha mabondia wengi
zaidi.
Mara tu baada ya kustaafu ndondi mwaka huo alianzisha klabu ya ndondi ya
Simba na kwa kuanzia akawachukua watoto wa mzee Ally Matumla Namwera; akina
Matumla, Haji, Rashid na Hassan, ambao hivi sasa wamekuwa maarufu katika mchezo
huo duniani kote.
Baadaye akawachukua akina Mbwana, Karim na
Mazimbo Matumla, Iraq Hudu, Joseph Marwa, Adeli Mkajanga, Oscar Manyuka,
marehemu Steven Bicco, Patrick Kibona, Shabani Mhamila 'Star Boy' , Adam
Abdulrahman, Maneno Oswald, Rajab Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa ni kocha wa
kimataifa wa mchezo wa masumbwi na ni msaidizi wake katika kuwanoa vijana
chipukizi kwa sasa, Abdallah Nyuni, Nassor Kondo, Rehema Matumla, Theresia
Kapinga, na wengineo wengi.
Enzi hizo mabondia nyota wa Afrika waliongozwa na Lottie Mwale na
Francis Musankabala (Zambia), Steven Muchoki, David Attan, Michael Irungu,
Robert Wangila, Isaya Ikonyi, na Modesti Napunyi (Kenya),
Wengine ni Emmanuel Mlundwa, Lucas Msomba, Ahmed Tesha, John Hugo,
Clemence Chacha, Isangura, Nassor Michael, Joseph Marwa, Onesmo Ngowi, Gerald
Isaac, Ali Muhamed, Emmanuel Kimaro, Rashid Matumla, Hamisi Kimanga na Koba Kimanga (Tanzania), Ayub Kalule,
John Mugabi, John Odhiambo, Boza Edward, John Byaruhanga, Mustafa
Waisaja na Cuban Businge (Uganda).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...