Na Bashir
Yakub
Baadhi ya wasomaji
wameuliza maswali mengi kuhusu
habari ya umiliki
wa mali kwa
wanandoa. Wanataka kujua ipi
mali ya ndoa
na ipi siyo, wanataka kujua mali
unayokuwa nayo kabla
ya ndoa inahesabika
vipi baada ya
kuingia nayo katika ndoa, wanataka kujua
uuzaji wa mali
za ndoa, wanataka
kujua kigezo kinachozingatiwa katika
kugawana mali ndoa inapovunjika, wanataka kujua
iwapo inawezekana kuwa na umiliki
wa pekee wa
mali wakati upo
katika ndoa, wanataka
kujua haki ya mali kwa
ndoa ya mke zaidi
ya mmoja, wanataka kujua
nani kati ya
mume na mke
ana haki zaidi
ya mali na
mengine mengi.
Haya yameulizwa na
watu tofauti lakini
kwa wingi. Hata hivyo mengi yake
yalikwisha elezwa hapa.
Mengi yameelezwa katika
makala tofauti zilizopita. Tunaamini
wapo walioona na
wengine hawakuona. Kwasababu hiyo
hakuna ubaya kujibu
tena maswali ya
aina hii ili
hata ambao hawakubahatika kusoma
waweze kusoma leo.
1.JE NDOA
INAPOVUNJIKA NI KIGEZO KIPI
HUTUMIKA KATIKA KUGAWA
MALI ZA WANANDOA.
Iliwahi kuelezwa hapa
kuwa wengi wanajua kuwa
katika kugawana mali
za ndoa pale
ndoa inapovunjika kigezo
kinachotumika ni cha
asilimia. Wanajua kwamba sheria
imeeleza wazi kuwa
kuna asilimia fulani
anatakiwa kupata mwanamke
na asilimia fulani
mwanaume.
Hili si
kweli kwani kigezo
kikubwa kinachotumika ni
kigezo cha nguvu au
juhudi za pamoja
katika upatikanaji mali( joint
effort) husika. Juhudi za pamoja
huangaliwa mchango wa kila
mmoja katika upatikanaji
au uendelezaji wa
mali husika.
Na juhudi za
pamoja sio tu pesa
au mali bali
pia hata kazi
za nyumbani nazo
ni sehemu ya
juhudi za pamoja
katika kupatikana kwa
mali.
Kwa hivyo juhudi ya kila
mmoja itapimwa na
mali zitagawanywa. Mahakama ndio
chombo chenye mamlaka
na kazi hiyo.
KUSOMA ZAIDI NENDA sheriayakub.blogspot.com



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...