Dkt. Ally Yahaya Simba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.

“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua  dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha kazi na watendaji wa serikali wakiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, pamoja na ma-Katibu wakuu Wizara ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora, Katibu Mkuu Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu Fedha na Mipango Mhe Dottoa James, Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na watendaji wengine. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. This step is long overdue. It come just too late. Miaka mingi mtu aki pigs simu Tanzania kutoka nje anayepokea nyumbani anakuuliza upo Dar es salaam? Ukiuliza kwanini unaambiwa namba inyoonekana huko ni namba ya Tigo, Airtel ama Voda! Maajabu sana. Kisha namba hiyo inayoonekana huko hata wewe mwenyewe huijui wala hujawahi kuitumia. Yule unayempigia akiipiga hiyo namba haipatikani!

    Binafsi nilishawaandikia TCRA kupitia msemaji wao hadi leo sina jibu. Nilialamika mbona duniani kote namba ya mpiga simu inaonekana upande wa pili isipokuwa Tanzania tu? Kumbe yote hayo yalikuwa ni mipango ya kuinyima Serikali mapato ya kodi za simu zinazopigwa toka nje ili kuonekana ni local calls! Hiyo ndiyo Bongo kweli!

    Hongera Magufuli.

    ReplyDelete
  2. TIMUA MAFISADI WOOTEE

    ReplyDelete
  3. Kweli Kabisa mdau namba mmoja hapo juu unayosema hata mie nakumbana ns hayo lia nikipiga simu toka ughaibuni naulizwa umeingia Tanzania lini maana wanaona namba ya ''Bongo'' wakati nipo diaspora.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora

    ReplyDelete
  4. Dr Magufuli uko sahihi sana kwani nchi ilishaingiliwa na mchwa tangu siku nyingi na tawala zilizopita zilikuwa dhaifu kwa hili.Endelea kusafisha mpaka mchwa wote waishe

    ReplyDelete
  5. duu kabla kuzima vimeo feki kazimwa yeye! hapa kazi tu

    ReplyDelete
  6. Hongera Rais na wote mnaofuatilia mapato ya Taifa kwa manufaa ya wananchi wote.

    Naomba serikali imtumie yule jamaa Shamte na wenginewo waliokamatwa kuonyesha ni jinsi gani hawa jamaa walikuwa wanafanya ujanja wa kukwepa kodi na jinsi walivyokuwa wanabadili namba za nje kuonekana za ndani. Pia ni kwa mda gani mambo haya yamefanyika.

    Hii mbinu inatumiwa na FBI kwa kuwashirikisha wahalifu ili waonyeshe njia kufichua mitandao yote ya haya maovu.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana sana Rais wetu Magufuli. Kaza kamba hadi uozo wote uishe. Wahusika wachunguzwe na vyombo husika na mali zirejeshwe serikalini, adhabu zinazoambatana na makosa haya zitolewe bila kusita. Lazima wote tufahamu kuwa trend imebadilika kuanzia awamu ya tano na kuendelea!

    ReplyDelete
  8. The mdudu, tumbua tumbua hapa kazi2 wengine na akili zao timamu eti ooh huu utumbuaji haufuati sheria eti sisi ni watu wa haki za kibinaadamu mlikua wapi wakati watanzania wakitaabika na kuteseka kutokana na hao wezi wa Mali za umma na Mafisadi? tunaomba mkae pembeni ili nchi isafishwe na Watanzania tuneemeke na Mali zetu za umma tumbua tumbua baba watanzania tuko nyuma yako wengine kwa kauli zenu mlisema mnajenga vyama vyenu vya kisiasa sasa nini tena mbona mnaacha kujenga hivyo vyama mnamlukia JPM alieamua kuijenga Tanzania yetu na kutokomeza umangi meza, umungu mtu, ufisadi, wizi, udokozi, upumbavu wa watu wachache wasioitakia mema Tanzania yetu na mengineyo ya kijinga Tanzania kwanza na hapa kazi2 wewe kama hupendi kuona Tanzania ikisonga mbele jiuwe sisi tutakuzika tu ila sisi tunachotaka kuona Tanzania ikisonga mbele

    ReplyDelete
  9. Nzuri Sana wezi wote wafunge watanzania wawe Wa kweli Kama tunataka maendeleo hawezi kuna juu mti kwa nini watu wajifunzi Mungu hibariki Tanzania na Rais wetu na watu wake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...