Benki ya NMB nchini imetoa vifaa vyenye thamani ya Tshs Millioni 28 kwa Klabu mpya nne za waandishi wa Habari nchini.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Desktop Computers 16, laptops 4 na printers 4 ambavyo tayari vimekabidhiwa kwa Geita Press Club na vinatarajiwa kuwasilishwa kwa Katavi Press Club , Simiyu Press Club, na Njombe Press Club ambapo kila klabu itapata Desktop Computer 4, Laptop 1 na Printer 1.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Desktop Computers 16, laptops 4 na printers 4 ambavyo tayari vimekabidhiwa kwa Geita Press Club na vinatarajiwa kuwasilishwa kwa Katavi Press Club , Simiyu Press Club, na Njombe Press Club ambapo kila klabu itapata Desktop Computer 4, Laptop 1 na Printer 1.
NMB imetambua kuwa ni muhimu kusaidia harakati za habari nchini kupitia kuwezesha klabu mpya za waandishi wa habari za mikoa mipya ya Geita, Simiyu, Katavi na Njombe.Huo ni msaada mkubwa kuwahi kutolewa kwa klabu za waandishi wa habari nchini, NMB imetambua umuhimu wa klabu za waandishi wa habari katika kutumia habari katika kusukuma mbele maendeleo ya nchi hii.
Akiongea katika makabidhiano ya vifaa vya Klabu ya Geita yaliyofanyika mwishoni mwa juma katika Ofisi za UTPC Mwanza.Mkurugezi Mkuu wa NMB Tanzania Ms. Ineke Bussemaker alisema kwamba wanautambua mchango Mkubwa wa UTPC katika sekta ya habari hapa nchini, hivyo baada ya kupokea maombi ya vifaa kutoka UTPC wakaona ni vyema kuwapatia vifaa hivyo, ili waandishi wa habari waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Mkurugenzi wa NMB - Ineke Bussemaker akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo. Kutoka kushoto waliokaa ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari wa Geita – Daniel Limbe, Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Bw. Abubakar Karsan na kutoka kulia ni Meneja wa NMB tawi la Kenyatta road na Meneja wa NMB kanda ya ziwa – Abraham Augustino.
Mkurugenzi wa NMB - Ineke Bussemaker akikabidhi rasmi kompyuta mpakato kwa Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Bw. Abubakar Karsan.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...