JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori – Mweka na Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)

Katika uteuzi huo, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Profesa Faustin K. Bee kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori MWEKA. na Profesa Apolinaria E. Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Uteuzi huo ni kwa kipindi cha miaka 
mitatu kuanzia tarehe 14/3/2016.

Kufuatia uteuzi huo uliofanywa na Mhe. Rais, Waziri wa Maliasili na Utalii kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Sura ya 209 kifungu cha 4(3) kikisomwa pamoja na Jedwali aya ya 2(1b) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori MWEKA kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia tarehe 14/3/2016.

Wajumbe walioteuliwa ni;
Samwel Maganga, Professor of Wildlife Management Sokoine University of Agriculture, Morogoro.Amani Ngusaru, Country Director, Tanzania World Wildlife Fund for Nature (WWF), Dar es Salaam.Andrew Gguga Seguya, Executive Director/CEO of Uganda Wildlife Authority, Kampala.Jafari Kidegesho, Department of Wildlife University of Agriculture Morogoro.Zuher H. Fazal, Vice Chairman Tanzania Tourism Organization, TATO, Arusha.

Alexander N. Songorwa, Mkuu wa Chuo cha Mweka, Moshi Simon Mduma, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania – TAWIRI, Arusha,Hassan Mshinda, Director General COSTECH, Dar es Salaam.Fred Manongi, Mhifadhi Mkuu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. – NCAA,Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi Tanzania -TANAPA, Arusha.Herman W. Keraryo, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii.

Aidha kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI Sura ya 260 kifungu cha 6(2) kikisomwa pamoja na Jedwali la 2 aya ya 1(c), Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia tarehe 14/3/2016:

Wajumbe wa walioteuliwa ni;
Ndelilio A. Urio, Profesa wa Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji Chuo cha Kilimo Sokoine, Morogoro.Martin Loibooki, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA.Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu, Hifadhi za Taifa TANAPA, Arusha.Freddy Manongi, Mhifadhi Mkuu, Mamlaka ya Hifadhi ya. Ngorongoro – NCAA Simon Mduma, Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI, Arusha.Theresia Nkya, Principal Medical Research Scientist NIMRI, Tanga. Revocatus Kurwijila, Professor of Food Science, Chuo cha Kilimo Sokoine Morogoro.
Hassan Mshinda, Mkurugenzi Mkuu, COSTECH, Dar es Salaam.Masound H. Mruke, Profesa, Idara ya Entomolojia na Nyuki, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Geophrey Kirenga, Katibu Mtendaji, Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania SAGCOT, Dar es Salaam.

IMETOLEWA NA:
Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi
KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tanzania ikishindwa kuendelea kwa uteuzi huu wa maprofesa basi tutakuwa tumelogwa. Nasikia mizigo bandarini imepungua. Ikiwezekana shusheni VAT ili wafanyabiashara waitumie kwa wingi.

    ReplyDelete
  2. Watanzania huwa tunakuwaga na matarajio potofu sana, mimi kama professor nipimwe ufanisi wangu katika umahiri wa kutafiti na uongozi wa shughuli za utafiti - researchers na pia ufanisi katika uandishi/publication ya utafiti. Uwezo katika utafiti sio na hauendani wala kufanana na uwezo na ufanisi na uongozi wa taasisi. La hasha hizi ni nyanja tofauti sana. Elimu kidogo kwa watanzania wataweza kutofautisha hili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...