Na Profesa Joseph Mbele
Mwaka huu, Song of Lawino, utungo maarufu wa Okot p'Bitek wa Uganda, unatimiza miaka hamsini tangu uchapishwe. Utungo huu, ambao unafahamika kama wimbo, ulichapishwa na East African Publishing House mwaka 1966 ukapata umaarufu tangu mwanzo.

Ulisomwa mashuleni na katika jamii kote Afrika Mashariki na sehemu zingine. Ulileta msisimko na upeo mpya katika dhana ya ushairi katika ki-Ingereza, na ulichochea washairi wengine kutunga kwa mtindo aliotumia Okot p'Bitek, ambao ulijaa athari za ushairi wa jadi wa ki-Afrika.
Siku chache zilizopita, niliandika katika blogu hii kuwa nimechapisha mwongozo wa Song of Lawino. Kitu ambacho sikusema ni kuwa nilikuwa na sababu ya kuchapisha mwongozo huu wakati huu, na sababu yenyewe ni hayo maadhimisho ya miaka 50.
Kwa kweli hiki kitabu ni kizuri sana sana sana! Song of Lawino and Ocol na Clementine ndani kwa kweli nakumbuka enzi hizo mtu unakisoma hiki kitabu, hata ukija kwenye kukihakiki inakuwa rakhisi zaidi maana kama vile umeangalia 'movie' tu, the way muundo, mtindo na mtiririko wa mashairi yake ulivyopangiliwa. Pongezi za dhati kwa mtunzi Okot p'Bitek from Uganda na pia Hongera na Pongezi za pekee kwa kutimiza miaka 50 tangu kutungwa kwa utungo huu wa 'Song Of Lawino'.
ReplyDelete