WAKALA wa ufundi wa umeme (TEMESA) wakaa kujadili namna bora ya kutengeneza, kuhudumia kutunza magari,pikipiki na mitambo ya Serikali.
Hayo yamesemwa na Kaimu mtendaji mkuu wa TEMESA, Mhandisi Manase Lekujan wakati akizungumza katika kikao cha maafisa wa usafirishaji wa wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa matengenezo ya magari, mitambo na pikipiki za serikali ni jukumu la TEMESA.
Manase mesema kuwa pamoja na kuwa na majukumu hayo pia wanatoa huduma za ushauri wa kiufundi katika maeneo umeme, mitambo, viyoyozi na majokofu serikalini.
Kaimu Mkurugenzi wa uzalishaji na matengenezo TAMESA, Mhandisi Sylivester Simfulave akizungumza na
maafisa wa usafirishaji wa wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali jijini Dar es Salaam leo.
Mhandisi, Elirehema Mmanry akizungumza katika kikao cha maafisa wa usafirishaji wa wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dr es Salaam leo.
Baadhi ya maafisa wa usafirishaji wa wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali wakimsikiliza mtoa maada katika kikao cha kujadiliana namna bora ya kutengeneza magari, mitambo na pikipiki za serikali jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...