Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara imepokea jumla ya madawati 500 kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Akiongea wakati wa kupokea madawati hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego alisema msaada huu unamaliza kabisa tatizo la madawati kwa kata zote za kijiji cha Madimba na Msimbati. Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema kwamba TPDC itaendelea kutoa misaada katika maeneo ambayo inafanya shughuli zake lengo likiwa ni kuboresha maisha wa wananchi wa maeneo hayo na kufaidika na shughuli za utafiti na uendelezaji wa gesi na mafuta. 
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akikabidhi rasmi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego na Mbunge wa Mtwara Vijijini. Mhe. Hawa Ghasia wakifurahia kwa pamoja baada ya TPDC kukabidhi madawati kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Madimba wakiwa wamekaa katika madawati waliyopokea kutoka TPDC.
Tpdc asanteni kwa kujali jamii ..miundo mbinu italindwa na sisi wote.asante
ReplyDelete