Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA), kutoka Tanzania, Mh.Abdullah Mwinyi, (katikati-wapili kulia), akipewa maelezo na meneja wa soko la samaki Ferry, Bw.Solomon Mushi, kuhusu biashara ya samaki sokoni hapo leo Aprili 20, 2016.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

WABUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania, wameendelea na ziara za kutembelea shughuli za kiuchumi za wananchi na leo Aprili 20, 2016 walikuwa kwenye soko la samaki la kimataifa ferry jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao wakongozwa na mwenyekiti wao, Mh. Makongoro Nyerere, Wamewaeleza viongozi wa wavuvi, wakaanga samaki na wapaa samaki fursa zilizopo kwenye ushirikiano wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki ambapo kwa sasa lina jumla ya nchi wanachama sita, Sudan Kusini ikiwa ndio mwanachama wa hivi karibuni kabisa.

Wabunge hao pia wametembelea na kujionea shughuli zihusianazo na samaki kwenye soko hilo. Pia walipata fursa ya kusikiliza maoni mbalimbali ya wadau hao katika soko la samaki Ferry. Soko lasamaki Ferry ni moja ya maeneo yanayotoa ajira kwa vijana wengi hapa jijini Dar es Salaam, ambao ukiacha wavuvi wao hufanya kazi ya kupaa samaki, kushusha samaki kutoka kwenye mitumbwi na kukaanga samaki. Pia kuna akina mama na baba wanaotoa huduma za chakula.
Mh. Mwinyi, akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana mawazo baina ya wabunge hao nawashika dau kwenye soko hilo, wengine kutoka kushoto ni Meneja wa soko hilo, Bw. Mushi, Mwenyekiti wa bodi ya soko ambaye pia ni diwani wa kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam, Mh.Masaba, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, na Mh. Nderaikindo Kessy
Mvuvi akieleza maoni yake mbele ya wabunge hao.
Shughuli za samaki zikiendelea kwenye moja ya mabanda ya soko hilo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivi hawa wabunge wao wanafanya nini? Mbona kutembelea tu kila siku? Ama Bunge hilo linaleta fedha ya kupanua soko? Tuelezwe basi.

    ReplyDelete
  2. siku watanzania watakapojua matumizi na haki ya kodi zao wenda hali ikawa nzuri.....ebu angalia soko lilivyo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...