Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Profesa Ndalichako alifungua mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa elimu Tanzania yaliyo fanyika katika chuo cha walimu Kleruu leo. waliojumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Sumbawanga, Songwe na Mbeya. 

Mafunzo hayo yana husu uhakiki wa ubora wa KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu). Akifungua mafunzo hayo Dr Ndalichako alisema serikali imepania kukuza ubora wa elimu inayo tolewa hivyo basi lazima itaboresha kitengo cha uhakiki ubora wa elimu Tanzania. 
Mkuu wa wilaya bwana Richard Kasesela akitoa salamu alisema " ni wakati muafaka kubadili KKK iliyopo iliyo zoeleka sasa yaani KULA, KULALA na KUCHEZA kuiirejesha kwenye maana halisi ya KUSOMA, KUANDIKA na KUHESABU.
Mkuu wa mkoa Bi.Amina Masenza akimkaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Ndalichako,Bi Masenza alimuomba waziri wa Elimu kuhakikisha Wahakiki ubora wanapewa kipaumbele katika kukuza elimu Tanzania.
Baadhi ya waliohudhuria mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa elimu Tanzania yaliyofanyika katika chuo cha walimu Kleruu leo. Mafunzo hayo yajumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Sumbawanga, Songwe na Mbeya. 
Sehemu ya meza kuu kwenye mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mh Ndalichako si DR ni PROF. HIVYO ANASTAHILI KUITWA MH PROF NDALICHAKO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...