Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii, Dar

Kocha mkuu wa timu ya Taifa'Taifa Stars'  Charles Boniface Mkwasa imetangaza kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya utakaopigwa Mei 29 jijini Nairobi.

Akitaja majina hayo kocha Mkwasa ameonekana akiwapa kipaumbele vijana huku akimrudisha Nadir Haroub 'Canavaro' na golikipa wa Yanga Deogratius Munish 'Dida'.

"Tumeamua kuangalia wachezaji wachanga na vijana hasa katika kujenga timu ambapo tunaweza kutumia mfumo wowote,"amesema Mkwasa.

Mkwasa amesema wachezaji hao walioitwa waliweza kufanya vizuri kwenye mechi zao katika ligi kuu na wameonyesha uwezo wa hali ya juu kwahiyo imani yake wanaweza kufanya vizuri.

 Wachezaji walioitwa ni magolikipa 3 Deogratius Munishi 'dida'(Yanga) Aishi Manula (Azam) Beno Kakolanya (Prison) mabeki ni AggreyMorris (Azam) Mwinyi Haji (Yanga) Mohamed Hussein (Tshabalala),Juma Abdul (Yanga) Erasto Nyoni (Azam)  Nadir Haroub 'canavaro' (Yanga) David Mwantika(Azam) na Vicent Andrew 'dante'  (Mtibwa)

Kwa upande wa viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba) ,  Jonas Mkude (Simba) ,Himid Mao (Azam) , Hassan Kabunda (Mwadui), Shiza Kichuya (Mtibwa)  Mohamed Ibrahim (Mtibwa) Ismail Juma (JKU) Farid Mussa (Azam) na Juma Mahadhi (Coastal Union)

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (Genk ubelgiji), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), Jeremia Juma (Prisons) Deus Kaseke (Yanga) Ibrahim Ajib (Simba) John Bocco (Azam) na Elius Maguli ( Stand United).

Mkwasa amesema kuwa wachezaji hao wanatakiwa kuingia kambini siju ya Jumatatu Mei 23 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuumana na Misri kufuzu mataifa Afrika AFCON Juni 04.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...