Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
  TIMU ya Abajalo imefanikiwa kutoka na ushimdi wa goli 3-2 dhidi ya The Mighty Elephant ya Songea na kufikisha alama 6 zitakazomruhusu kuvuka hadi ligi daraja la kwanza. 

 Abajalo ndio walioanza kufunga dakika ya 10 kupitia kwa Ally Saidi ambaye amefunga mawili na bao jingine dakika ya 77. 

 Waziri Omary akaipatia timu yake goli kwa mkwaju wa penati huku magoli ya The Mighty Elephant yakifungwa na Simon Minga na Raymond Lwambano dakika ya 46 na 90. 

 Kufuatia matokeo hayo Abajalo wameungana na Mvuvumwa wenye alama 6 sawa nao na kuweza kupanda hadi ligi daraja la kwanza  baada ya timu ya Pamba kuwa na alama 4 huku The Mighty Elephant akisalia na alama 1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...