Na Zainab Nyamka
MABINGWA wa ligi kuu bara na wawakilishi wa michuano ya kimataifa timu ya Yanga imefanikiwa kuvuka hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho baada ya kuwaondoa GD Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya goli 2-1.
Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Sagrada Esperanca mjini Dundo umemaliza kwa GD Sagrada Kutoka na ushindi wa goli 1-0 lakini wameshindwa kuvuka hatua hiyo baada ya mechi ya awali Yanga kushinda 2-0 wakiwa nyumbani.
Kutokana na matokeo hayo, Yanga wameingia hatua ya makundi wakiungana na TP Mazembe pamoja na Etoile Du sahel huku mechi zingine zikiwa zinaendelea kuchezwa.

Mchezo huo ulioanza saa 11 jioni kwa saa za  Afrika Mashariki umemalizika huku beki wa Yanga na nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub 'canavaro' akitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 82 lakini juhudi za golikipa Deogratius Munish 'dida' aliweza kuokoa penati katika dakika za nyongeza na kuifanya mechi hiyo kumalizika kwa Yanga kufuzu hatua ya makundi
Mechi hiyo ilijaa vurugu sana na mpira kuchezwa takribani dakika 100 huku Sagrada wakitafuta goli la kusawazisha,huku wachezaji wa Yanga Thaban Kamosoku, Amisi Tambwe na Dida wakipewa kadi za njano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...