Meneja wa Airtel Money, Asupya Nalingigwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa huduma ya MR. MONEY ambayo itaendeleza kurahisisha matumizi ya huduma ya kifedha kupitia simu za mkononi kwa uhakika katika kufanya miamala mbalimbali kwa gharama nafuu na kuhakikisha muamala wako unakamilika kwa usalama kabisa.
amesema kuwa huduma ya Airtel Money Tap Tap ni huduma nyingine inayowasaidia wateja wakeinayotoa nafasi kwa wateja kufanya malipo kupitia kadi maalumu bila kuwa na haja ya kuwa na simu ya Mkononi.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kifedha kwa njia ya mtandao wa simu wa Airtel huduma ya MR. MONEY.
Mkuu wa Kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa udiznduzi wa huduma ya MR.MONEY jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa huduma ya MR. MONEY inawezesha wateja wake kupata mkopo ya Timiza isiyo na harama kwa wateja na mawakala wa Airtel Money.
Amesema kuwa wateja wa Airtel wanaweza kununua Luku na kupewa muda unit nyingine za ziada endapo mteja akitumia airtel Mone kununua Umeme. usikose kupata nafuu ya fedha zako unapomtumia pesa wapendwa wako kwa kutumia Artel Money bila gharama yoyote.
Kwa kutumia huduma mbalimbali za MR. MONEY piga *150*60# kufurahia huduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...