Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa 'Taifa Stars' Nadir Haroub 'Canavaro' amesema kuwa hatoweza kuichezea tena timu ya Taifa kwani ameshaandika barua kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) ya kustaafu kuchezea timu hiyo.

Canavaro ameamua kusema hivyo baada ya kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kumuita tena kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu kwenye mechi alizocheza.
"Nimeshaandika barua TFF ya kuwaambia kuwa nimestaafu kuchezea timu ya Taifa na wanafahamu sasa kuitwa kwangu tena mimi siwezi kujiunga hata kama wakiniomba,"amesema Canavaro.
Naweza kukubali kujiunga na timu yangu ya Taifa kama viongozi wa Yanga watanisihii kwenda lakini kwa upande wangu naendelea na msimamo.
Canavaro amejitoa kwenye majukumu ya kitaifa baada ya kuvuliwa unahodha bila taarifa kitu kilichopelekea kuamua kujiweka kando akionesha ni kitendo cha dharau alichofanyiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...