Umoja wa wanawake Tanzania Mkoa wa Arusha Wilaya ya Arusha mjini wamefanya uchaguzi ili kumpata mwenyekiti wa (UWT) katika wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa (UWT) Mkoani hapa Flora Lazaro Zelothe, amesema kuwa lengo la uchaguzi huo ni kumpata mwenyeketi wa umoja wa wanawake Wilaya ya Arusha mjini na kuongeza kuwa watu wenye maslahi binafsi hawawahitaji bali watu wenye mapenzi mema na umoja huo.
Flora amewataka wanawake kuacha makundi kwani yamekuwa yakiwatenganisha na hayana faida yeyote zaidi yakubomoa ,Bali wafanye kazi kwa bidii nakujituma kwa kushirikiana na viongozi wao,ili kuleta mafanikio katikaumoja huo.
Mary Kissaka baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Arusha Mjini.

Baada ya kutangangazwa kuwa mshindi kwa kura 319, Bi Mary Kissaka amewashukuru wanawake kwa kumchagua kwa kumpa kura za heshma,na ameahidi kwamba atawatumikia UWT.Kuanzia ngazi Tawi, Kata ,hadi Wilaya kwa kushirikiana na wanawake.
Ameongeza kuwa Aatafanya ziara kila tawi ,ili kufanya tathmini ya uhai ya wanachama, ili kila mwanachamaaweze kulipa ada ya mwaka kwa wakati, Pia amesema kwa ataanzisha miradi mbalimbali kwa kushirikiana na UWT.
Sambamba na hilo amewashauri wanawake wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zinapojitokeza kwani wanaweza, na amewataka kuzitumia nafasi hizo vizuri ili kuleta maendeleo katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...