VIWANDA VIPYA KUJENGWA ILI KUKABILIANA UPUNGUFU WA SUKARI.Na Tiganya Vincent, Dodoma.
Serikali inaendelea na mazungumzo na wawekezaji wanaokusudia kuwekeza katika viwanda vya sukari ili kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini.Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya papo kwa papo ya kila Alhamis.
Alisema kuwa lengo la mazungumzo ya kutaka viwanda viweze kuongeza uzalishaji wa sukari ili uweze kufikia tani 420,000 katika kipindi miaka minne ijayo na hivyo kupunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.Mhe. Majaliwa alisema kuwa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vipya ya Sukari ni pamoja na Kigoma, Morogoro na Bonde la Rubada lilipo katika mto Rufiji.
Kuhusu kutojengwa kiwanda cha Sukari katika eneo la Bagamoyo , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ilikataa kuruhusu ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika eneo hilo baada ya Kamati ya Bunge kushauri kuwa kisijengwe kwa sababu kingehatarisha uhai wa wanyama waliomo katika Mbuga ya Saadan kwa kuwa kingetumia maji mengi kutoka Mto Wami.
Mhe. Majaliwa alisema kuwa hali hiyo ingesababisha upungufu wa maji ambayo ni tegemeo kwa wanyama wa Mbuga ya Saadan yambao ni muhimu kwa sekta ya utalii nchini.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...