Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(katikati) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, Jijini Mbeya akiwa ameongozana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia). Kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Adamu Mambi. Katibu Mkuu anatarajia kesho Mei 20, 2016 kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza katika Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akisalimiana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Mbeya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Camir Minja.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira kesho tarehe 20 Mei, 2016 saa 3:00 asubuhi anatarajia kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili katika Chuo cha Magereza, Kiwira Mkoani Mbeya.
Mafunzo hayo ambayo yamechukua muda wa miezi mitatu yalilenga kuwaandaa Maafisa(pichani) kuwa viongozi wa kati katika vituo vya Magereza nchini. Jumla ya wahitimu ni 327, kati yao Wanaume 246 na Wanawake 81, Aidha Wanaume 08 na Wanawake 02 wanatoka Vyuo vya Mafunzo Zanzibar.
Sherehe hizo, zitajumuisha mambo yafuatayo:-
* Mgeni Rasmi kukagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na wahitimu hao;
* Mgeni Rasmi kutoa vyeti kwa Wanafunzi waliofanya vizuri katika Mafunzo ya darasani na
Mafunzo ya mbinu za medani;
* Mgeni Rasmi kuvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kwa wahitimu wawili kwa niaba
ya wahitimu wengine na;
* Mgeni Rasmi kutoa Hotuba.
Sherehe za ufungaji wa Mafunzo hayo zinatarajia kukamilika saa 8:00 mchana. Vyombo vya Habari vinakaribishwa
kwenye sherehe hizo siku ya Ijumaa tarehe 20 Mei, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA
Mei 19, 2016




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...