Rose
Mdami
Wadau kutoka Sekta mbalimbali nchini leo
wamekutana katika kongamano maalumu kujadili suala la Vitambulisho vya Taifa na
uwezekano wa kukamilika kwa mradi huo ili kuwezesha taifa kuwa na
Kanzidata(database) yenye taarifa sahihi zenye kujibu maswali makuu nini ni
nani, yuko wapi na anafanya nini. Lengo ni kurahisha utoaji huduma na kuwezesha
wananchi kujishughulisha na masuala ya biashara kwa kuwa na mfumo rasmi
unaowatambua
Akifungua kongamano hilo, Kaimu Gavana wa Benki
Kuu ya Tanzania, Dkt. Nato Mwamba amesema mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu
ni mfumo ambao umesubiriwa kwa siku nyingi kwani manufaa yake ni makubwa katika
mifumo mbalimbali nchini hususani mfumo wa biashara na taasisi za fedha nchini
Amesema kutokana na kupanuka kwa matumizi ya
teknolojia nchini, huduma nyingi zikiwemo huduma za kifedha zinategemea sana
kuwepo kwa mfumo wa Vitambulisho vya Taifa ili kuwezesha watu wengi zaidi
kunufaika na huduma zitolewazo kwa sasa kwani wengi wanakwama kwa kuwa hakuna
mfumo rasmi unaowatambua.
Mafanikio ya mfumo huu ni kufungua milango kwa
wananchi wengi zaidi kunufaika na huduma mbalimbali zinazoendelea kutolewa
nchini zikiwemo huduma za kifedha na hivyo kuwataka wadau hao kuwezesha NIDA
kufikia malengo ya usajili nchi nzima kufikia Disemba 31, 2016 ili mfumo wa
Utambuzi wa Taifa uweze kuunganishwa na mifumo mingine
Akieleza mkakati wa usajili kufikia Disemba 31,
2016, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dkt. Medestus Kipilimba amesema NIDA
imejizatiti kutumia taarifa za zilizokusanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
kuanza usajili utakaowezesha wananchi waliosajiliwa katika daftari la wapiga
kura kuhakikiwa na kupata usajili awamu ya kwanza ambao utahusisha namba ya
utambulisho kabla ya kupata kitambulisho cha Taifa.
Amesema hatua ya kufanya
usajili wa awali na kutoa namba ya utambulisho itawezesha wananchi kuanza
kufaidi utambulisho wao kwa kuwawezesha kupata huduma mbalimbali. Hata hivyo
ili mwananchi kupata utambulisho kamili lazima kukamilisha hatua za usajili kwa
kuhakikisha anawasilisha nyaraka muhimu za utambuzi ili kuendelea kupata huduma
nyingine
Kwa mara ya kwanza NIDA itaanza kuzalisha
vitambulisho vyenye saini ya mwombaji ambayo itawekwa kwenye uso wa mbele wa
kitambulisho na nyumba ya kitambulisho kutakuwa na saini ya mtoaji. Amesema
hatua zote katika kukamilisha mpango huo zimekamilika
Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau toka Taasisi
za fedha nchini, TASAF, Wamiliki wa makampuni ya simu nchini, Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania, Benki ya Dunia (World Bank), SSRA, BIMA, Melinda and Bill
Gates Foundation, Tanzania Bankers Association( TBA) na wawakilishi wa Taasisi
mbalimbali za Serikali.
Naibu Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akifungua kongamano la wadau kuhusu vitambulisho vya Taifa lililofanyika leo katika ukumbi wa Benki Kuu na kuhudhuriwa na wadau toka sekta mbalimbali nchini
Mkurugenzi mtendaji wa Financial Sector Deepening Trust Sosthenes Kewe akichangia mada wakati wa kongamano wa wadau lililohusu mpango wa Usajili vitambulisho vya Taifa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Dkt. Modestus Kipilimba akionyesha wadau sampuli ya vitambulisho vyenye saini vitakavyoanza kutolewa hivi karibuni, wakati wa kongamano la wadau kuhusu mpango wa vitambulisho vya Taifa
Mr. Sanjay C. Rughani Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini akiwasilisha mada wakati wa kongamano la wadau katika mpango wa usajili vitambulisho vya Taifa
Mkurugenzi wa Fedha toka TASAF Bw. Joshua Nyamko akiwasilisha mada katika kongamano la wadau kujadili Vitambulisho vya Taifa
Baadhi wa washiriki wa Kongamano la wadau kuhusu mpango wa Usajili vitambulisho vya Taifa wakisikiliza kwa makini mada ya mkakati wa Usajili kufikia Disemba 31,2016 iliyowasilishwa na NIDA.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...