Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo leo Bungeni mjini Dodoma 19 Mei, 2016.
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Andrew Chenge (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Mhe. Cecilia Paresso wakielekea ndani ya Bunge kwa ajili ya Vikao vya asubuhi vya bunge hilo 19 Mei, 2016 mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya asubuhi katika Bunge hilo leo 19 Mei, 2016.
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (mwene gauni la kitenge) akiwa na baadhi ya Wabunge wakielekea ndani ya bunge kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya bunge hilo 19 Mei, 2016 mjini Dodoma. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA. MAELEZO, DODOMA.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...