Miradi yote ya
maendeleo nchini Tanzania kuhifadhiwa kwenye kanzi data ili kurahisisha uratibu,
upembuzi, ufadhili na utekelezaji wake.Kituo cha kuchakata na
kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na
kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.
Akiongea katika
ufungunzi wa mkutano wa kupata maoni ya taasisi za serikali zinazotekeleza
miradi ya maendeleo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bi. Florance
Mwanri alisema uwepo wa taarifa za miradi zitasadia taifa.
“Uwepo wa kanzi data
hii utakuwa na manufaa sana kwa taifa kwa sababu itakuwa ni rahisi kufanya
maamuzi katika mchakato mzima wa kutekeleza miradi” alisema Bi. Mwanri.
Miongoni mwa faida
zitakazo tokana na mfumo huu ni kurahisisha upatikanaji wa vipaumbele vya
miradi, kufanyika kwa upembuzi yakinifu vilevile upanikanaji wa fedha za
kufadhili miradi hiyo. Pia mfumo huu utarahisisa utekelezaji na ufuatiliaji wa
miradi iliyoidhinishwa na serikali.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Florance Mwanri
akifuatilia utangulizi wa mapendekezo ya
uundaji wa mfumo wa utunzaji wa miradi ya maendeleo – Kanzi data (Data Base),
kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Omar Abdallah.
Bi. Salome Kingdom akichukua taarifa za mapendekezo ya wadau
mbalimbali ya kutoka taasisi za serikali ili kuboresha uundwaji wa wa kanzi
data hiyo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mjadala.
Kaimu Naibu Katibu Mtendaji – Uzalishaji, Bi. Lorah Madete,
akielezea jinsi taifa litakavyonufaika na mfumo huu. Kushoto kwake ni Bi.
Zena Hussein na Bw. Hekima Chengula ambao ni sehemu ya kamati ya maandalizi.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Florance Mwanri
akiteta jambo na wataalamu kutoka Tume ya Mipango kuhusu mrejesho wa mkutano
huo.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...