Na Teresia Mhagama, Geita
Imeelezwa kuwa Ruzuku ya Awamu ya Tatu inayolenga katika kuendeleza shughuli za uchimbaji mdogo wa madini nchini itatolewa mwezi Septemba mwaka huu.
Hayo yamesemwa mjini Geita na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa kikao kilichojumuisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Alisema kuwa hivi karibuni alizungumza na Benki ya Dunia ambayo imeahidi kutoa Dola za Marekani kati ya Milioni 3 na Milioni 4 ambazo zitatolewa kwa vikundi mbalimbali vya wachimbaji wadogo nchini.
Aliongeza kuwa fedha hizo zitatumika pia kuendeleza vituo Saba vya mfano vya utafutaji na uchimbaji mdogo wa madini ambavyo vitachaguliwa na Wizara baada ya kufanya tathmini ya maeneo yanayoweza kuwekwa vituo hivyo. “Maeneo hayo Saba ya mfano yatafanyiwa utafiti na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) ili kufahamu mashapo ya dhahabu yaliyopo katika eneo husika kabla ya kuyagawa kwa wachimbaji wadogo,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema kuwa Wanawake waliopo katika shughuli za uchimbaji mdogo wa madini, ukataji na uchongaji wa madini ya Vito pia watafaidika na Ruzuku hiyo lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wanawake wanaojishughulisha na sekta ya Madini nchini.
“Tunatafuta Ruzuku hizi ili ili wachimbaji wadogo mpande daraja na kwenda kwenye uchimbaji wa kati ambao utaleta tija kwenu na kwa Taifa kwani uchimbaji huu huwa hautikisiki pale bei ya dhahabu inaposhuka duniani kwani gharama za uzalishaji kwenye migodi ya kati ni za chini tofauti na migodi mikubwa,”alisema Profesa Muhongo.
Aidha aliwaeleza wachimbaji wadogo nchini kujiunga katika makundi yatakayowawezesha kupata Ruzuku hiyo kwani haitatolewa kwa mtu mmojammoja na kuwaasa kushirikiana na Idara inayosimamia Wachimbaji Wadogo katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili kuweza kuandika maombi ya kuomba Ruzuku husika.
Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeendelea kutoa Ruzuku katika Uchimbaji madini mdogo ambapo katika mwaka wa Fedha 2015/16 zilitengwa takribani Shilingi bilioni 7.2 ambazo zilitolewa kwa vikundi 111 vya wachimbaji wadogo na watoa huduma mbalimbali katika sekta ya uchimbaji madini mdogo.

Vilevile, katika mwaka wa Fedha 2013/2014, Fedha za Ruzuku zilizotolewa kwa Wachimbaji Wadogo zilikuwa ni Dola za Marekani 500,000 sawa na takribani Shilingi Bilioni 1 zilizotolewa kwa waombaji 11.
Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Leseni, Mhandisi John Nayopa (katikati), Meneja wa TANESCO Kanda ya ziwa, Mhandisi Amos Maganga (kulia) na Mhandisi Joseph Kumburu (kushoto) wakiwa katika kikao kilichofanyika mjini Geita kilichojumusha watendaji mbalimbali katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Kikao kililenga kujadili suala la magwangala na maeneo ya Wachimbaji Wadogo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kulia) na Katibu Tawala mkoa wa Geita, Selestine Gesimba (kushoto) wakiwa katika kikao kilichofanyika mjini Geita kilichojumusha baadhi ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Geita, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika Kikao kilichofanyika mjini Geita ambacho kililenga kujadili suala la magwangala na maeneo ya Wachimbaji Wadogo kilichoongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (hayupo pichani).
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kushoto) na Katibu Tawala mkoa wa Geita, Selestine Gesimba (kushoto kwa Mkuu wa Mkoa) katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa, kabla ya kufanya kikao kilichojumusha baadhi ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilicholenga kujadili suala la Magwangala na Maeneo ya Wachimbaji Wadogo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...