Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela amedhuria kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Iringa na kutoa rai kuhakikisha waheshimiwa madiwani wanabuni mbinu mpya za kukusanya mapato zisizo waumiza wananchi, mfano gereji ya manispaa ingeweza kutumika kukagua magari kwa kushirkiana na polisi.
Katika hotuba yake alisisitiza suala la Ulinzi na usalama hasa ulinzi wa Mtoto na mama, kwani sasa imekuwa kawaida wanaume kupiga wake zao na kukosa utu. Pia watoto wana bakwa lakini taarifa hazifiki kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, zile zinazo fika ziapungikiwa ushahidi.
Mheshimiwa Kasesela amesitiza suala mipango miji endelevu yenye kufikiria mbali zaidi, nyumba zote ambazo hazifai kwa makazi wahusika waambiwe. Vichochoro vyote vilivyofungwa vifunguliwe ili kuondoa hali hatarishi.
Kwa upande wa elimu alitoa Msistizo mkubwa kwa kila diwani ulikuwa kuhakikisha kila shule inakuwa na madawati ya kutosha.
Baraza hilo lilifunguliwa na Mstahiki meya Mh. Alex Kimbe, pia alikuwapo Naibu meya Bwana Nzala Lyata, Mbunge wa Iringa mjini mh Peter Msigwa. Madwani walijadili mapendekezo ya vikao vya kamti mbalimbali na kupitisha maazimio yote.
![]() |
| Mstahiki meya Mh Alex Kimbe akifungua baraza |
Mkuu wa wilaya Iringa Mhe. Richard Kasesela akitoa rai kwa Manispaa ya Iringa kuongeza kasi ya kukusanya mapato
Mh Peter Msigwa akichangia hoja
Mh Leah Mleleu Diwani viti Maalum (CHADEMA) akisiliza kwa makini
Mh Nyalusi akichangia hoja







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...