Na  Bashir  Yakub.
Katika  saa  za  kazi  zipo  saa  za  kazi  katika  siku  za  kawaida, saa  za  kazi za  ziada   na  saa  za  kazi  katika  siku  ambazo  ni  za  sikukuu. Kuna  umuhimu  mkubwa  sana  kwa mfanyakazi  kujua  masaa  ya  kazi  . Kama  hujui  masaa  ya  kazi  ya  kisheria  basi ni  vigumu  kujua   usahihi  wa  ujira  unaolipwa .
 Malipo  ya  kazi  hayatokani  na  mshahara  pekee. Yapo  malipo  mengine  ya  ziada  yatokanayo  na  muda  wa  ziada zikiwemo  siku  za  sikukuu. Ili  ujue  usahihi  wa  kile  unacholipwa yakupasa  kujua pia mchanganuo  wa masaa  ya  kazi.  Masaa  ya  kazi  yapo  aina  mbili.
 Yapo  masaa  ya  kazi  ya  kawaida  na  yapo  masaa  ya  kazi  ya  ziada. Sikukuu  nazo  hujumuishwa  katika  masaa  ya  kazi  ya  ziada.

1.JE  SAA  ZA  KAZI  NI NGAPI KATIKA SIKU  ZA  KAWAIDA  ?.
Katika  siku  za  kawaida  saa za  kazi  ni 9.  Kwahiyo kwa  siku  mfanyakazi  anatakiwa  kufanya  kazi  masaa  9. Hii  ina  maana  atafanya  kazi  masaa   45 kwa  wiki ikiwa atafanya kazi  kuanzia jumatatu  mpaka ijumaa.
Muhimu  sana  katika  suala la  saa  za  kazi  ni  kuwa  mfanyakazi asifanye  kazi  zaidi  ya  saa  45 kwa  wiki kwa masaa  ya  kawaida.Hata  siku  zikizidi  lakini  masaa  45  kwa  wiki  yasipite. Hayo  ni  masaa  ya  kawaida.
2.  JE  SIKU  ZA  KAZI  NI NGAPI ?.
Siku  za  kazi  zinazoruhusiwa  ni  sita  kwa  wiki. Lakini  itategemea na  taratibu  za  ofisi  yako. Zipo  ofisi  watakwambia tunafanya kazi   jumatatu  mpaka  ijumaaa  na  wapo  wengine  watakwambia  kazi  ni  jumatatu  mpaka  jumamosi. Hawa  wote  watakuwa hawajakosea  kwasababu  bado  wako  ndani  ya  ukomo  wa  siku  za  kisheria.
Linalopaswa  kuzingatiwa  hapa  ni  kuwa  vyovyote  itakavyokuwa  masaa  ya  kazi  kwa  wiki  yasizidi  45.  Iwe siku  tano  kwa wiki au  sita  muhimu masaa  yasizidi  45  kwa  wiki.  Haya  ni  masaa  ya  kawaida.  Masaa  ya  kawaida  ni  yale masaa  ambayo  sio  ya  ziada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2016

    Inakuwaje saa 9 za kazi kwa siku wakati tunafanya kazi saa 1.30 mpaka 9.30? Ukipiga mahesabu inakuwa saa 8 kwa siku. Na hii ni hata kwa wale wanaofanya kazi saa 2 mpaka 10.

    Jumla ya masaa kwa wiki yatakuwa ni 40 na siyo 45. Kwa kawaida jumamosi haimo isipokuwa kwa kazi maalumu za ziada, au nimekosea?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...